Na Scholastica Njozi – Law School of
Tanzania
Waziri wa Katiba na Sheria, Prof.
Palamagamba Kabudi amewataka watumishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa
Vitendo Tanzania (Law School) kutambua kuwa wamebeba dhamana kubwa kwa
Taifa.
Waziri Kabudi ametoa wito huo leo
alipotembelea Taasisi hiyo wakati akiwa katika ziara ya kutembela taasisi
zilizo chini ya Wizara hiyo ili kujionea namna Taasisi hiyo inavyotoa mafunzo.
“Nataka niwahakikishie kuwa mmebeba
jukumu kubwa sana kwa Taifa hivyo mnapotekeleza majukumu yenu zingatieni sana
kuhakikisha wahitimu wanakuwa na maadili, wasiopenda rushwa na kubwa zaidi
watambue wanakwenda kuwatumikia watanzania maskini”, alisema Mhe. Waziri.”
Prof. Kabudi aliongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria,
Amon Mpanju.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Taasisi
Dkt. Zakayo Lukumay, amesema watahakikisha wahitimu wote wanakuwa na uzalendo
kwa nchi yao kwa kupitia mafunzo wanayoyapata.
Prof.
Palamagamba Kabudi mwenye tai nyekundu akiwa na viongozi wa Taasisi
alipotembelea majengo.
Prof. Palamagamba Kabudi, akimsaidia mwanafunzi Bi. Jesca Mbawala namna ya kutafuta vitabu
kupitia mtandao, alipotembelea maktaba ya Taasisi.
Waziri wa Katiba na Sheria, Prof.Palamagamba Kabudi akitia saini kitabu cha wageni
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...