Meneja Miradi Airtel Tanzania Jane Matinde akizungumza wakati wa semina kwa vijana kuhusu
umuhimu wa kusoma kwa kutumia mtandao kupitia aplikesheni ya VISOMO inayotumiwa na
VETA kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel iliyofanyika makao makuu ya
kampuni hiyo Morocco, Dar es Salaam jana.
Baadhi ya washiriki wa semina kwa vijana kuhusu umuhimu wa kusoma kwa kutumia mtandao
kupitia aplikesheni ya VISOMO inayotumiwa na VETA kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel wakifuatilia kwa umakini mafunzo yaliokuwa yanatolewa kwa ajili ya
kuwahamamisha jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Magilatech Company Ltd. Godfrey Magila na mtaalamu wa
tenklojia akitoa mafunzo kwa vijana waliodhuria semina kuhusu umuhimu wa kusoma kwa
kutumia mtandao kupitia aplikesheni ya VISOMO inayotumiwa na VETA kwa kushirikiana na
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Morocco, Dar
es Salaam jana.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikia na VETA leo wametoa mafunzo kwa
vijana mkoani Dar itakayowawezesha kuongeza ujuzi na kuenda sambamba namahitaji ya soka
la ajira na kujiajiri.
Mafunzo hayo yenye lengo la kutoa fursa mbalimbali zinazopatikana kupitia ushirika wa watoa
huduma hao yanalenga katika kuwawezesha vijana nchnini kujiendeleza kielimu kupitia
application ya VSOMO kwa kupata masomo ya ufundi stadi ya VETA kupitia simu zao za
mkononi ili kuongeza ujuzi wao.
Akiongea wakati wa semina hiyo , Meneja Mradi wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema
Tumeonelea vyema kufanya semina hii ili kuongeza uelewa kwa vijana juu ya fursa hii
muhimuinayotoa nafasi ya kijana kujitambua na kujiajiri mwenyewe mara baada ya kusoma
masomo ya Ufundi kupitia simu zao za mkononi na kupata cheti. Tunao vijana Zaidi ya wateja
30,000 ambao wamepakua application ya VSOMO kati yao 9,000 wamejiandikisha ili kusoma
kwa mtandao lakini idadi ya waliopata vyeti bado ni chache, hivyo tumeonelea ni vyema kujikita
katika kutoa elimu na kuwahamashisha watanzania kutumia technologia hizi za kisasa
kujisomea wakati wowote mahali popote kupitia simu zao za smartphone na hatimae kufanya
mafunzo ya vitendo na kupata cheti.
Tunatoa wito kwa watanzania hususani vijana kuchangamkia fursa hii kwa kupakua application
ya VSOMO kwenye simu zao na kusoma kozi hizi za ufundi ambazo gharama yake ni
120,000/= hadi kumaliza na kupata cheti.
Kwa upande wake mtaaalamu wa technologia na Mkurugenzi wa Magilatech Company Ltd. Bw,
Godfrey Magila alisema, Techonologia inakuwa kwa kasi sana ni muhimu kutumia Tehama
katika kuleta tija katika kibiashara, kilimo , elimu na kadhalika. Kwa kuona hivyo tumeanzisha hii
application ya VSOMO ambayo ni ya kwanza dunia kutoa mafunzo ya ufundi kupitia simu na
Tanzania tunajivyunia kupiga hiyo muhimu.
Naye Meneja Mradi wa VSOMO VETA , Bwana Charles Mapuli alisema, Ushirikiano wetu na
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kunaongeza wito katika kutoa elimu ya ufundi na
kuwafikia watanzania wengi Zaidi. Napenda kuwahakikishia kuwa masomo haya ya VETA
kupitia simu yamehakikiwa na VETA kuhakikisha yanatolewa katika ubora na viwango
vinavyotakiwa, na hivyo natoa wito kwa watanzania kutumia fursa hii kujiendeleza. Lengo letu
ni kuhakikisha kila mtanzania anapata fursa ya kujiendeleza na kuwa na ueledi
utakaomuwezesha kuajiriwa au kujiajiri.
Kozi zinazopatikana katika application ya VSOMO ni pamoja ni Huduma ya chakula na mbinu
za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta,umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa
Majumbani, Umeme wa magari. Vilevile Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi
wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi
wa kuchomea vyuma.


Tafadhali tunaomba ushirikiano wa usomaji wa vitabu mbalimbali vikilenga upande wa afya.
ReplyDeletewww.tovl.ac.tz