Kamati ya Sheria katiba na hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF wamemfungulia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja iliyokua inamkabili mchezaji Pius Buswita ambaye alifungiwa kutokana na kusaini mikataba miwili na timu za Yanga na Simba.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari asubuhi ya leo Mwenyekiti wa kamati hiyo Wakili Elias Mwanjala amesema Simba,Yanga na Mchezaji mwenyewe wamekubaliana Pius Buswita alipe pesa alizochukua katika klabu ya Simba wakati akisaini mkataba wa makubaliano ya kuichezea klabu hiyo.

Wakili Mwanjala amesema kilichofanywa na klabu hizo mbili ni busara tu ili kumpa nafasi mchezaji huyo acheze kinyume cha hapo mchezaji huyo angeendelea kutumikia adhabu yake na walichokitaka Simba wao ni kulipwa tu pesa zao ili kuondoa lalamiko hilo na mchezaji mwenyewe ameahidi mbele ya kamati kwamba atalipa.

Kiasi cha milioni 10 pamoja na gharama zingine ikiwa ni pamoja na usafiri na malazi ambazo kwa pamoja zinafikia milioni 1 ndizo zilizotajwa na Simba kwenye barua yao waliyoiwasilisha TFF na ndicho kiasi ambacho Yanga na mchezaji wameahidi kulipa na kamati imetoa onyo kali la kimaandishi kwa mchezaji huyo na ataruhusiwa kucheza tu iwapo Simba watathibitisha kulipwa pesa zao.

Buswita mchezaji wa zamani wa Mbao FC ya Mwanza alijikuta akifungiwa na shirikisho la soka nchini baada ya kusajiliwa na Yanga huku pia akiwa amesaini mkataba na Simba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...