Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

MKUU wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama, amesema anachukizwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimtolea maneno machafu ovyo, Rais Dk. John Magufuli hususan kwenye mitandao ya kijamii suala ambalo linaumiza.

Aidha amelaani vikali vitendo vya matukio ya baadhi ya watu kuwavamia na kuwashambulia kwa risasi viongozi. Pamoja na hayo ,Assumpter hakusita kukemea tabia ya utekaji wa watoto na kisha kupoteza maisha yao ikiwemo tukio lililotokea wiki iliyopita huko Kongowe Kibaha.

 Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na matukio yanayoendelea katika maeneo mbali mbali  alisema, anasikitishwa kuona vitendo kama hivyo vinaendelea kufanyika katika jamii ya watanzania hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kwa wananchi na baadhi ya viongozi kuishi  wakiwa katika hali ya hofu.

Assumpter alisema kuwa baadhi ya watu kwa sasa  wamekuwa wakiamua kumtolea maneno machafu kiongozi wa nchi bila ya kufahamu kuwa ni kinyume cha sheria na taratibu za nchi. Alieleza vitendo na tabia kama hiyo haifai hata kidogo katika jamii na badala yake watanzania wanatakiwa kuwa wazalendo na nchi yao.

Assumpter alibainisha kwamba, Rais Magufuli anafanya mambo Makubwa tangu kaingia madarakani na kupigania maslahi ya nchi. Alisema kikubwa ni kumuunga mkono na sio kumkebehi na kumtolea maneno machafu ambayo hata nchi na mataifa mengine watabakia kutushangaa.

"Rais Magufuli anapambana na wabadhilifu, raslimali za taifa ikiwemo madini na maslahi ya taifa kijumla "

Assumpter alisema, fedha nyingi zilikuwa zikipotea mikononi mwa baadhi ya watumishi wasiowaminifu ambapo yeye ameweza kurejesha mapato, kodi na fedha za wananchi zilizokuwa zikiliwa na wachache kwa maslahi ya matumbo yao.

“Nachukizwa sana na kuona matukio mbali mbali yaiendelea hapa nchini, kama vile watoto kutekwa nyara, baadhi ya viongozi kupigwa risasi kwa kweli hii sio sahihi huku wengine kutoa maneno machafu kwa kiongozi wetu wa nchi kwa hili mimi nalaani vikali"

“Napenda kuchukua fursa hii pia kumpa pole mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu kwa kuvamiwa na kushambuliwa na risasi za moto  na kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana"

"Huyu Tundu Lissu ni kiongozi mkubwa na ni mtu maarufu Tanzania lakini kitendo cha kushambuliwa na risasi sio kizuri na mimi namwombea kwa mungu apone na arudi kuendelea na majukumu yake ya kuwatumikia wananchi wa jimbo lake,”alisema Assumpter .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...