Na Freddy Macha
Sarakasi ni kati
ya sanaa hatari na za kusisimua sana. Kwa sasa Ulaya wapo vijana na watu wa makamo
mbalimbali waliohamia toka Afrika
Mashariki (hasa Kenya na Tanzania) wakitumbuiza
kadamnasi kwa sarakasi, Uingereza, Ureno, Ujerumani na Hispania.
Nchini Hispania
kuna visiwa vya Grand Canary ambapo Watanzania wachache hurukaruka kuvutia
maelfu ya watalii.
Moja yake ni Lanzarote. Hapa Mtanzania Mohammed Idi Mohamed aliyehamia baada ya kuishi Ujerumani kwa kipindi. Mohdy,
Muddy au Modi (mwenye rasta fupi pichani) aliwahi pia kufanya kazi Tanzania, Ureno na
Uingereza.
Alifariki Jumatatu
18 Septemba, 2017, asubuhi. Sababu za kifo chake zimeelezwa na waganga ni
kuvuja damu kutoka mfereji wa koo kwenda mapafu na kutokea tumboni.
Alipasukwa
mshipa huu wa damu ghafla na kuanguka
bafuni akipiga mswaki. Bahati nzuri Muddy alijikatia bima ya maisha ambayo
imeondoa tatizo la kusafirisha mwili wake nyumbani kuzikwa. Michango
iiliyoombwa kutolewa itasaidia familia yake na gharama nyingine za mazishi. Tuma kupitia Western Union. Huwa bei
nafuu zikitumwa zifike kesho yake badala ya siku hiyo hiyo... Marehemu ameacha
watoto wawili na wajukuu. Mungu aiweke roho yake pema peponi.
Kwa walio
Ujerumani, ni Malimbo Saidi Malimbo, simu (+49 ) 1522-4082848.
Uingereza, Saidi
Kanda (+44) 4040-66607. Tanzania, Eddy Sengo,
(+255) 656 210 725.
Picha ihsani ya
Fab Moses, Lanzarote, Hispania
-London, 26 Septemba 2017
-Bpepe: gmacha52@gmail.com
-Tovuti: www.freddymacha.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...