Jalada la kesi la utakatishaji wa fedha inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Wakili wa Serikali  Mkuu, Vitali Peter aliyaeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.
Ameeleza kuwa  hadi sasa bado wanasubiri kurejeshwa kwa jalada hilo na maelekezo kutoka kwa DPP ili aendelee na kesi kama atakuwa amejiridhisha na uchunguzi kuwa umekamilika.

Kufuatia taarufa hiyo, wakili wa utetezi, Evodius Mtawala ameiomba mahakam kutoa ahirisho fupi kwa sababu taratibu za kiofisi haziwezi kuchukua muda mrefu.

 Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 4,2017.

Aveva na makamu wakw Kaburu  wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...