MAREHEMU CASSIUS O. MDAMI
Tangu umetuacha tumetafakari mengi tukidhani umesafiri utarudi lakini
kumbe haikuwa hivyo. Kuwa kwako mbali na familia kumetufanya kujifunza
mengi kuhusu maisha na kutafakari muda ambao tulikuwa pamoja katika
maisha ya hapa duniani wakati wa furaha na uchungu. Unakumbukwa na mke
wako Rose na watoto wako Martina, Grace, Gideon, Gonsalver na Gibson.
Umetimiza mwaka sasa tangu umetuacha; pengo lako ni kubwa katika kila
kona ya maisha na hata katika Tasnia ya Habari uliyoitumikia katika muda
mwingi wa maisha yako kwa kutuonyesha kwa vitendo maana ya kuipenda na
kuithamini kazi katika maisha.
Tumekosa simulizi za kusisimua za Utalii wa
Ndani, ulichimba na kuchimbua mengi ambayo kama si kwa jitihada zako
binafsi tusingeyajua kamwe… tumebaki na msemo wako maarufu “Falsafa ya
Ufagio ni Unyenyekevu”.
Faraja yetu ni Mungu aliye Baba wa Yatima na
mume wa Wajane (Kutoka 22:22-24). Tunaamini katika Ufufuo na Uzima na
siku moja tutafurahi nawe mbinguni (Yohana 11:25-26).
Mungu akupe
pumziko la Milele, upumzike kwa Amani - Amina
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...