Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imesema October 4 mwaka huu, itatoa uamuzi kama Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu(Pichani) anayekabiliwa na kesi ya uchochezi ana kesi ya kujibu au la.

 Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa amesema hayo leo baada ya upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi kufunga ushahidi wao kwa kuita mashahidi watano.

Kabla ya hayo, Lissu alidai kuwa, kwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ameona kabisa kuwa hana kesi ya kujibu. Hata hivyo, Hakimu Mwambapa amesema ni jukumu la Mahakama kuamua kama mshtakiwa anakesi ya kujibu au la.
Aidha Mahakama imezitaka pande zote mbili, ile ya mashtaka na ya utetezi Septemba 18, kuwasilisha hoja zao kama mshtakiwa ana kesi ya kujibu au la.

Katika kesi hiyo, Lissu anakabiliwa na kesi ya uchochezi ambapo mapema mwaka huu, akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alitoa kauli za uchochezi kuwa, “Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, “huyu diktekta uchwara lazima apingwe kila sehemu”. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...