Maryam Kidiko na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar.
KUANDALIWA kwa kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ni miongoni mwa juhudi za kuendeleza lugha ya Kiswahili katika ukanda huo na Duniani kwa jumla.
 Hayo ameyasema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki huko katika ukumbi wa  Hoteli ya Golden Tulip iliopo Malindi Mjini Zanzibar.
 Alisema kongamano hilo lililowashirikisha wataalamu wa lugha ya Kiswahili wa nchi wananchama wa Afrika Mashariki  lina umuhimu mkubwa katika historia ya maendeleo ya Kiswahili duniani pamoja na kupanga mikutano na kubadilishana utalaamu .
  Hivyo Alieleza kuwa ni muhimu kwa kamisheni kusimamia kwa makini hadhi ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano ikitambuwa kwamba ukanda wa Afrika Mashariki ni sehemu ya Dunia yenye lugha tofauti.
 Samia alisema uratibu na uendelezaji wa Maendeleo na matumizi ya Kiswahili utaimarisha mchakato na utengamano wa Jumuiya kwa maendeleo endelevu. “Utengamano wa Jumuiya sio tukio bali ni mchakato ambao unapaswa kuendeshwa na watu wenye kuelewa vizuri matumizi endelevu ya Kiswahili “Alisema Makamo wa Rais.

04  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwaonyesha wajumbe walioshiriki  Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki mpango mkakati wa miaka mitano wa Kamisheni hiyo (kulia) Mtendaji Mkuu wa Kamisheni Prof. Kenneth Simala na (kushoto) Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...