Mfanyabiashara Yusuph Manji, akitoka Mahakamani baada ya Hakimu Mkazi, Huruma Shahidi kuruhusu yeye na wenzake watatu wanaokabiliwa na tuhuma za uhujumu uchumi kupelekwa polisi kuhojiwa ili kukamilisha upelelezi.






HABARI KAMILI;..................
Na Karama Keyunko,Blogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, imeruhusu mfanyabiashara Yusuf Manji na wenzake watatu kupelekwa polisi na kuhojiwa dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili ili kukamilisha upelelezi.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi kufuatia barua ya maombi kutoka kwa Mkuu wa upelelezi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, (ZCO), ndipo akaandika hati ya kuwatoa washtakiwa mahabusu (remove order) ili kuwafanyia mahojiano katika kesi namba 33/2017

Amesema hawawezi kukataa maombi hayo ya polisi kwani kufanya hivyo ni sawa na kupingana na kauli ya mahakama ya kukamilisha upelelezi, na ndio maana ikatolewa hati ya kuwatoa mahabusu kwa ajili ya mahojiano. “Hii sio mara ya kwanza kuwatoa washitakiwa kwa upelelezi," alisema Hakimu Shaidi.

Aidha amewaagiza polisi kuhakikisha washtakiwa wanatendewa ikiwemo kuzingatia afya zao kwani wanawakabidhi wakiwa na afya nzuri na kama watahitaji uwakilishi wa mawakili wao wapate uhuru wa kuwakilishwa kwenye jambo lolote na isiwe kificho.

Hakimu Shahidi amesema, "Namkabidhi Koplo Dotto kama barua inavyoelekeza kuwa nimkabidhi Sajenti Mkombozi au Doto lakini kwa kuwa Mkombozi hayupo basi namkabidhi Doto ila washitakiwa warudishwe kesho ndani ya muda wa kazi.

Mbali na Manji, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda (28), Mtunza stoo, Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43)  mkazi wa Chanika wanakabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi.

Mapema, akiwasilisha maombi hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi aliiomba mahakama iruhusu washitakiwa waweze kukabidhiwa kwa Polisi ili kutimiza matakwa ya upelelezi ambapo amedai kifungu
Cha 59 cha CPA kinawapa mamlaka Polisi kufanya upelelezi.

Hata hivyo, wakili wa utetezi Hudson Ndusyepo alipinga watuhumiwa kwenda kuhojiwa kwa madai kuwa, mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri hiyo sababu DPP hajatoa Kibali kwa mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo zaidi ya kutaja tarehe, alidai mahakama hiyo imefungwa mikono ya kutoa amri dhidi ya maombi hayo au yoyote yale.

Naye wakili Hajra Mungula aliiomba mahakama kukataa ombi hilo kwa madai kuwa washitakiwa hao wako chini ya ulinzi na kwamba upande wa mashitaka uliwashitaki washitakiwa kwa mbwembwe na kuwasilisha hati ya kuwazuia dhamana huku wakijua kwamba hawajakamilisha upelelezi

Hata hivyo, Wakili Kishenyi alidai mahakama imekuwa ikisisitiza kukamilisha upelelezi na kwamba wanachofanya ni sehemu ya kukamilisha upelelezi.
Pia alidai washitakiwa hao wanahaki ya kuwakilishwa hivyo maombi yao yakubaliwe.

Washtakiwa hao wanadaiwa kukutwa na sare za na vifaa mbali mbali vya jeshi.
Mfanyabiashara Yusuph Manji, akitoka Mahakamani baada ya Hakimu Mkazi, Huruma Shahidi kuruhusu yeye na wenzake watatu wanaokabiliwa na tuhuma za uhujumu uchumi kupelekwa polisi kuhojiwa ili kukamilisha upelelezi.

Manji aliyeletwa mahakamani hapo kwa hati ya kuwatoa mahakamani (remove order) anaenda kuhojiwa kufuatia barua ya maombi mahakamani hapo kutoka kwa ZCO, pia mahakama imewaamuru kesho kabla ya muda wa kazi kuisha wawe wamerudishwa mahakamani hapo.

Mbali ya Manji washtakiwa wengine ni Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere.

Manji na wenzake hao wamekabidhiwa kwa Detective  Koplo Dotto ambaye ametakiwa mpaka kesho ndani ya saa za kazi wawe wamerudishwa mahakamani.

habari kamili itafuata baadaye kidogo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...