MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanya uwekezaji wa Dola za kimarekani  Milioni 3.90 katika kiwanda cha machinjio  na usindikaji nyama cha Nguru ‘Nguru Hills Ranch Limited’ kilichoko nje kidogo ya Morogoro Wilaya ya Mvomero.

Akizunguza katika  uwekaji wa saini kwenye mkataba wa uwekezaji, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga, alisema uwekaji wa saini umefikiwa baada ya tathini ya kina iliyofanywa na mfuko huo.Alisema mfuko umejiridhisha  kuhusu usalama wa rasilimali za wanachama kwenye uwekezaji huo.

“Tunatambua kuwa Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji katika viwanda lakini LAPF imeona fursa hii ni moja wapo ambayo inakidhi vigezo vyote vya ajenda ya uwekezaji”alisema Sanga.

Alisema LAPF imewekeza kwenye kiwanda hicho kwa ubia na kampuni ya ‘Eclipse Investments LLC’ inayotokana na kampuni tanzu ya Zubair Corporation ya Oman na kampuni ya ‘Busara Investments LLP’ na kufanya wabia kuwa watatu.

“Kiwango cha uwekezaji kilichofanywa na LAPF ni USD 3.9 Milion ambayo ni sawa na asilimia 39 ya hisa za kampuni,ambapo Eclipse Investments LLC inaa hisa asilimia 46 na Busara Investments LLP ina hisa asilimia 15”alisema  Sanga.

Alisema kiwanda hicho kina ukubwa wa ekari 6,000 ambapo ekari 1,200 zimejengwa miundombinu ya malisho ya mifugo kwa kipindi kisichopungua siku 90 kwaajili ya kuwanenepesha na kuwapa ubora kabla ya kuchinjwa.

Sanga alisema kiwanda hicho kitakuwa na uwezo kuchinja na kuchakata ng’ombe 300 na mbuzi 2,000 kwa siku na kusafirishwa mara moja.

“Nyama itakayozalishwa kwa kiwango kikubwa itasafirishwa nje kwenye nchi za mashariki ya kati na mashariki ya mbali ambako soko ni kubwa na Oman”alisema Sanga.

Alisema kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja 500 na nyingine zisizo za moja kwa moja na kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya viwanda vingine.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga (wa pili kushoto), akisaini mkataba wa makubaliano ya uwekezaji katika Kiwanda cha Machinjio ya kisasa na Usindikaji Nyama cha Nguru Wilayani Mvomero.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga (wa pili kushoto), akibadilishana hati na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zubair Corporation ya Oman, C.S. Badrinath, baada ya kusaini makubaliano ya uwekezaji katika machinjio ya kisasa ya Nguru.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Clliford Tandari (katikati), akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni wa LAPF, Eliud Sanga, baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya uwekezaji katika Kiwanda Machinjio ya kisasa na Usindikaji Nyama.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa Uwekezaji katika Kiwanda cha Machinjio ya kisasa na Usindikaji wa Nyama cha Nguru 'Nguru Hill Ranch Ltd' kilichopo Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Zubair Corporation ya Oman, C.S.Badrinath na katikati ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Clliford Tandari.
 Baadhi ya wadau walioshiriki katika hafla hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...