KAMPUNI ya Udalali ya Msama, imetangaza msako wa wezi wa kazi za sanaa kwa ujumla wake ambao wamekuwa kikwazo cha wahusika kutofaidi matunda ya ubunifu, jasho na kazi zao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama alisema kazi hiyo ngumu na muhimu kwa maslahi ya wasanii na Serikali, inaa siku yoyote kuanzia sasa.Msama alisema kutokana na wizi huo kuwanyonya wasanii pamoja na kuikosesha Serikali pato lake halali kupitia kodi, kampuni yake imepewa jukumu hilo kwa msaada wa Jeshi la Polisi.
“Naishukuru Serikali kwa kusikia kilio cha wasanii mbalimbali kuanzia wale wa muziki wa injili, Dansi, Bongo Fleva na hata  wengineo, wamekuwa wakilia kazi zao kutajirisha wajanja,” alisema Msama.Msama alisema kibaya zaidi ni kwamba, wizi huo wa kazi za sanaa  sio tu umekuwa ukiwanyonya wasanii, pia ni kuinyima Serikali mapato halali kwa ajili ya kuzitumia kwa maendeleo ya nchi.

Alisema kazi hiyo itakayofanywa na kampuni yake kwa ushirikiano wa karibu zaidi na Jeshi la Polisi, utagusa mikoa yote ya Bara kwa kukamata wote wenye kuuza kazi zisizotambulika kisheria. “Hii ni pamoja na kazi zote zisizo na stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hivyo wenye kuuza CD, DVD feki pamoja na kunyonya kazi za wasanii katika flash, wote hawatabaki salama,” anasema.

Alisema ni heri wenye kujihusisha na kazi hiyo haramu, wakatafute kazi nyingine halali kwani tayari wanayo majina, hivyo wanajua waanzie wapi siku na saa ya kuanza kutoka mkoa mmoja hadi mwingine.“Tunatangaza kuwa, tunaingia kazini kusaka wote wenye kujipatia vipato kutokana na ubunifu na jasho la wengine, huku wahusika wakibaki masikini. Msako huu hautaacha mtu,” alionya Msama.

Mbali ya ukurugenzi mkuu katika kampuni hiyo ya Udalali, Msama pia ndiye mdau aliyechangia kukua kwa muziki wa injili kupitia uratibu wa matukio ya Tamasha la Pasaka, Krismas ama uzinduzi wa kazi mpya. Alisema katika hatua ya awali, msako huo utakaokuwa chini ya Polisi wapatao 100 katika maeneo mbalimbali ya nchi, utaanzia jijini Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma.
2
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake leo,jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...