Taarifa iliyotufikia hivi punde, inaeleza kuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Mawakili cha Tanganyika (TLS), Mhe. Tundu Antipus Lissu ameshambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani kwake Area D mjini Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu. 
Habari kutoka Dodoma zinasema Mhe. Lissu amepelekwa Nairobi kwa ndege maalum kwa ajili ya matibabu zaidi.
Kupitia mtandao wa Twitter, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza masikitiko yake dhidi ya tukio hilo, na kumuombea kwa Mungu Mhe. Lissu aweze kupona haraka huku akiviamuru vyombo vya ulinzi na usalama viwasake waliohusika na tukio hilo la kinyama na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...