Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amepewa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) ikiwa ni alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Akikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa AWAMATA Taifa, Mwenyekiti wa AWAMATA Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo amesema Asasi hiyo imehamasika kutoa tuzo ya cheti kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa sababu ni mzalendo na amekuwa akifikiri juu ya maendeleo ya wananchi na namna mbalimbali za kuzalisha ajira kwa vijana.
Amesema Mhe.Mtaka ni moja ya viongozi wabunifu sana na kama kiongozi kijana amekuwa na maono makubwa yenye manufaa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Taifa kwa ujumla, ambapo amehamasisha uanzishwaji wa viwanda katika Mkoa kupitia Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” na Kilimo cha Umwagiliaji wilayani Busega.
“Mhe.Mtaka tumeanza kumfuatilia toka akiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Wilaya ya Hai mpaka na baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, tumekaa kama asasi tukashawishika kumpa tuzo hii, kwa sababu amekuwa anafanya kazi ya kizalendo na maendeleo hasa anapoumiza kichwa kwa ajili ya kutengeneza ajira; tena kila wilaya kwenye mkoa wake ina kitu cha kufanya” alisema Golyo.
Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka, tuzo ya cheti kwa niaba ya Mwenyekiti wa UWAMATA Taifa, ambayo imetolewa kwa Mkuu huyu wa mkoa kama alama ya kutambua kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akionesha tuzo ya cheti aliyokabidhiwa na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Kutoka kulia Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka, Katibu wa AMAWATA mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Millensasha Mneo na Afisa Uhusiano wa AWAMATA, Ndg Shushu Joel wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi tuzo ya cheti iliyotolewa kwa Mhe.Mtaka kama alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa AWAMATA na wadau wengine wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kukabidhiwa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...