WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles John Mwijage ameaomba wawekezaji wa viwanda wa nchini India waje hapa nchini kuwekeza kwenye sekta za viwanda.
Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Pia amewaomba wakulima wa kilimo cha mbaazi za aina mbalimbali walime kwa wingi ili kuendana na soko la nchini India ambapo nchini Kwao zao hilo ni lulu kwao.
Pia amewaomba wataalum wa Kompyuta kutoka nchini India kuja hapa nchini ili kubadilishana uzoefu na watanzania hapa nchini.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles John Mwijage akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo akiwaaomba wafanyabiashara na wakulima wa mbaazi hapa nchini kuzilima kwa wingi ili kuliteka soko la nchini India. Pia amewaomba wawekezaji wa nchini india waje wawekeze hapa nchini ili kukuza ushirikiano wa kibiashara kati ya India na wafanyabiashara hapa nchini.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles John Mwijageakizungumza jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kutoka nchini china.
Amewasihi wawekezaji hapa nchini wawekeze katika viwanda vya kubangua korosho ili kurahisisha ubanguaji wa korosho hapa nchini ili kutimiza ndoto ya Tanzania ya Viwanda hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...