WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa vyerehani 25 kutoka katika Taasisi ya African Releaf Organization ya nchini Kuwait.

Amepokea msaada huo leo (Ijumaa, Septemba 9, 2017) kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Ruangwa.

Waziri Mkuu ameishukuru taasisi hiyo kwa msaada huo wa vyerehani ambavyo vitagawiwa kwenye vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wilayani Ruangwa.Amesema vyerehani hivyo vitawawezesha wajasiriamali wanaojishughulisha na ushonaji kupata vitendeakazi vitakavyotumika kama njia ya kujiongezea kipato.

Waziri Mkuu amesema mbali na kutoa msaada huo wa vyerehani pia taasisi hiyo inajenga Zahanati katika kijiji cha Mbecha kata ya Nanganga wilayani Ruangwa.“Taasisi hii ni rafiki na Halmashauri yetu na Wanaruangwa wamefarijika kwa kupata zahanati na vyerehani vitakavyotumika kama njia ya kujiongezea kipato.”

Awali, Mkurugenzi wa Miradi wa Taasisi ya African Releaf Organization, Bw. Khamis Mkanachi alishukuru kwa ushirikiano wanaoupa kutoka Halmashauri ya Ruangwa.Pia Bw. Mkanachi amesema taasisi yao itaendelea kuvisaidia vikundi mbalimbali vya ujasiriamali katika Halmashauri hiyo kwa lengo la kuvikwamua kiuchumi.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alimtembelea na kumpa pole mbunge wa jimbo la Newala Vijijini, Bw. Rashidi Akbar aliyelazwa katika Taasisi Moyo ya Jakaya Kikwete.Kwa upande wake Bw. Akbar alimshukuru Waziri Mkuu kwa kumtembelea hospitalini hapo na kwamba hali yake kwa sasa inaendelea vizuri ukilinganisha na alivyofikishwa.

Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kumjulia hali Bw. Anzigar Kambanga ambaye ni mwananchi wa wilaya ya Ruangwa aliyelazwa katika Taasisi Moyo ya Jakaya Kikwete.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, SEPTEMBA 9, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipeana mkono na mkurugenzi wa taasisi ya African Relief Organization, Wakati akipokea cherehani ikiwa ni sehemu ya vyerehani 25 vya msaada, zilizo tolewa kwa Wananchi wa Ruangwa kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Septemba 8, 2017, (kulia) ni Mratibu wa miradi wa African Relief Organization Bw. Khamis Mkanachi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...