Na Mathias Canal, Dar es salaam
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A.
Mwalimu leo Septemba 4, 2017 amezindua Ugawaji wa vitambulisho vya awali
7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo Jijini Dar es salaam.
Akizungumza
katika uzinduzi huo uliofanyika katika Viwanja vya TP Sinza E Waziri
Ummy alipongeza uongozi wa Wilaya ya Ubungo kwa kutambua umuhimu wa
kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali ya kuwatambua Wazee katika
Halmashauri na kuwapatia vitambulisho vitakavyo wawezesha kupata Huduma
za matibabu bila vikwao.
Alisema
kuwa Wazee ni asilimia 5.6 ya wananchi wote wa Tanzania idadi ambayo
kwa kiasi kikubwa inaleta msukumo wa nchi kuweka mifumo madhubuti ya
kuhudumia Wazee ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa Huduma katika
matibabu.
Alisema
kuwa Jambo hilo ni kuzingatia ukweli kwamba Wazee wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali zinazosababishwa na umri mkubwa na mtazamo wa
Jamii ambao umekuwa ukichangia ukiukwaji wa haki na maslahi ya Wazee
katika ngazi mbalimbali.
Alisema
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeingia kwenye rekodi kwa kuwatambua
Wazee wasio na uwezo kwani watapatiwa vitambulisho vitakavyo wawezesha
kupata Huduma za matibabu Bure.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...