MKUU
wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi ameuomba uongozi wa Vicoba Endelevu
hapa nchini kuhakikisha wanatanua mtandao wao uweze kuwafikia wananchi
wengi zaidi wakiwemo walimu, wafanyakazi wengine wa serikali pamoja na
wafanyabiashara ndogo ndogo ili kuisaidia serikali kufanikisha adhma
yake ya kuyakomboa makundi hayo kiuchumi.
Hapi alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati akizundua taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu iliyopo Bunju wilayani humo.
“Niwaombe sana viongozi wa Vicoba mtanue zaidi mtandao wenu ili muwafikie maelfu zaidi ya wafanyabiashara ndogo ndogo, wafanyakazi mbalimbali wa serikali wakiwemo walimu na mshirikiane nao katika kuangalia namna bora zaidi ya wao kupata huduma za kifedha ikiwemo mikopo ili waongeze thamani ya mitaji yao,’’ alisisitiza.
Zaidi, alitoa wito kwa wakina baba wahakikishe wanahamasisha wake zao pamoja na mabinti zao waweze kushiriki katika Vicoba ili kuinua vipato vya familia zao.
“Mbali na wakina mama pia hebu tuwahamasishe zaidi wasichana ambao wamekuwa wakitumia muda na pesa zao katika urembo na kujipodoa na badala yake sasa wajenge utamaduni kujijenga kiuchumi zaidi kwa kushiriki katika vikundi hivi vya kijasiliamali pamoja na Vicoba,’’ alisema.
Awali akitoa taarifa ya hali Vicoba endelevu hapa nchini, Rais wa Vicoba Endelevu nchini Bi Devotha Likokola alisema mtandao huo tayari unahusisha vikundi zaidi ya laki moja vikiwa na wanachama zaidi ya milioni mbili na laki mbili huku wakiwa na akiba ya zaidi ya Tsh Trilioni moja na milioni mia mbili.

MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi (alievaa suti nyeusi) akikata utepe wakati akizundua taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu yenye maskani yake Bunju wilayani humo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Rais wa Vicoba Endelevu nchini Bi Devotha Likokola (alieshika kipaza sauti) na Mkurugenzi wa Taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu Bi Semeni Gama (kulia kwa DC Hapi).

MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi (alievaa suti nyeusi) akikagua baadhi ya bidhaa zinazoandaliwa na wajasiliamali ambao ni wananchama wa Vicoba Endelevu baada ya kizundua taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu yenye maskani yake Bunju wilayani humo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi (alievaa suti nyeusi) akiongoza maandamano ya wajasiliamali ambao ni wananchama wa Vicoba Endelevu kuelekea kwenye ofisi za taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu yenye maskani yake Bunju wilayani humo jijini Dar es Salaam ambapo alizindua ofisi hizo mwishoni mwa wiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...