Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefungua mafunzo ya “Tathmini ya Uwezo” kanda ya Shinyanga ikiwa ni jitihada inayofanywa na shirika la Twaweza kwa lengo la kupima uwezo wa watoto juu ya umahiri wao wa kusoma,kuhesabu na kuandika.
Mafunzo hayo yanayofanyika kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga,yameanza leo Alhamis Oktoba 5,2017.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo,Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akisema washiriki wa mafunzo hayo ni waratibu wa wilaya na waratibu wa vijiji kutoka wilaya nane za kanda ya Shinyanga inayojumuisha mikoa ya Dodoma,Singida,Simiyu na Shinyanga.
“Mafunzo ya tathmini ya Uwezo yanafanyika nchi nzima na kwa upande wa kanda ya Shinyanga,yanafanyika hapa ambapo tunafundisha mbinu na taratibu za kufanya wakati wa kutekeleza zoezi la Tathmini ya Uwezo kwenye wilaya mbalimbali nchini Tanzania na mwaka huu zoezi litafanyika katika wilaya 56”,alieleza Mgoi.
Alisema washiriki wa mafunzo hayo watafundishwa namna ya kufanya tathmini kuhusu uwezo wa watoto wenye kuanzia miaka 6 hadi 16 katika masomo matatu ya Kiingereza,Kiswahili na Hesabu.
Aliongeza kuwa Twaweza kupitia tathmini ya uwezo imekuwa ikishirikiana na serikali katika kuboresha elimu nchini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo amefungua mafunzo ya “Tathmini ya Uwezo” kanda ya Shinyanga katika ukumbi wa Karena Hotel leo Alhamis Oktoba 5,2017-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akielezea kuhusu Tathmini ya Uwezo
Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akizungumza ukumbini.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...