
Mahafali haya yatatanguliwa na siku ya
utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao katika mwaka wa masomo
2016/2017, sherehe ambazo zitafanyika Ijumaa, tarehe 15 Desemba, 2017.
Taasisi inapenda kuwataarifu wahitimu
wa Shahada ya Uzamili (M.Eng) na Shahada ya Kwanza (B.Eng/BTech), kusoma utaratibu
na hatimaye kuthibitisha ushiriki wao katika Mahafali hayo kupitia tovuti ya Taasisi (www.dit.ac.tz)
Wahitimu watakaoshiriki wanapaswa kulipia
joho la Mahafali Tsh. 50,000/= (kwa wahitimu
wa Shahada ya Uzamili) na Tsh. 30,000/=
(kwa wahitimu wa Shahada ya Kwanza katika tawi lolote la NBC kwenye akaunti namba 018101003145
na hatimaye kujisajili kupitia tovuti ya Taasisi www.dit.ac.tz).
Watakaoruhusiwa kushiriki Mahafali
haya ni wale tu watakaokamilisha usajili wao.
ZINGATIA:
Malipo yafanyike kwa
kutumia jina kamili kama linavyoonekana kwenye orodha ya wahitimu wa mwaka 2016/17
iliyopo kwenye tovuti ya Taasisi, namba ya usajili na madhumuni ya malipo yaani
Mahafali.
Kwa wanafunzi wa Stashahada (OD)
ambao hawatavaa majoho wanatakiwa kuvaa nguo safi, nadhifu na zenye staha. Na hawa wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kupitia
tovuti ya Taasisi (www.dit.ac.tz) bila kulipia gharama zozote.
“Rehersal” itafanyika Alhamisi, tarehe
14 Desemba, 2017.
Mwisho wa kujisajili ni tarehe 15 Novemba, 2017.
Atakayeona tangazo hili anaombwa kumjulisha
mwenzake.
Tangazo hili limetolewa na:
Ofisi ya
Uhusiano,
Taasisi
ya Teknolojia Dar es Salaam,
S.L.P
2958,
Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...