Na Benny Mwaipaja, Dodoma
MAKAMU
wa Rais Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN, amezinduzi Sera ya Taifa ya Huduma
Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika
kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, tukio
litakalofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
Makamu
wa Rais ametoa wito kwa watoa huduma ndogo za fedha kupunguza riba za
mikopo na tozo mbalimbali ili kufanikisha lengo la Sera hiyo ambalo ni
kuimarisha huduma jumuishi za fedha kwa kujenga mazingira wezeshi
yatakayoleta ufanisi wa utoaji wa huduma ndogo za fedha nchini kwa
wananchi wenye kipato cha chini.
“Ninawaomba
pia muongeze ubunifu katika kutoa huduma zinazohitajika na wananchi wa
kipato cha chini pamoja na kupeleka huduma hizo katika maeneo yaliyo
karibu na makazi yao au biashara zao” aliongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan
Alizitaka
taasisi za huduma za fedha kuwaelimisha wananchi kabla ya kutoa huduma
hizo ili kupunguza athari wanazozipata wananchi.“Ni
matarajio yangu kuwa, Wizara ya Fedha na Mipango itashirikiana na wadau
katika kutekeleza Sera hii na kuhakikisha malengo ya Sera ambayo ni
kukuza uchumi na kupunguza umaskini yanafikiwa” alisisitiza
Alisema
Ripoti ya Finscope ya mwaka 2017 ambayo iilionesha kuwa Tanzania
imepiga hatua kwenye suala zima la huduma jumuishi za fedha (financial
inclusion) na kufikia asilimia 72 kwa 2017, huku changamoto kuu
iliyoainisha ni elimu/uelewa mdogo wa huduma za fedha kwa wananchi.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizundua rasmi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, mjini Dodoma.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania –TPB Bw. Sabasaba Moshingi baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, Mwenyekiti wa Kikundi cha Akiba na Mikopo-(KIKOBA) cha Mwende Manispaa ya Dodoma, Bi. Bertha Chisawilo, baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akimpongeza Mwenyekiti wa Kikundi cha Akiba na Mikopo-(KIKOBA) cha Mwende, Manispaa ya Dodoma, Bi. Bertha Chisawilo, baada ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, kumkabidhi Mwenyekiti huyo, Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...