Jumla ya wananchi 600 wameshiriki katika zoezi la upimaji wa magonjwa ya Moyo ambao ulienda sambamba na utoaji wa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani iliyofanyika tarehe 29/09/2017 katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
Wananchi walioshiriki katika zoezi hilo walipimwa urefu, uzito, shinikizo la damu (BP), sukari na kupewa ushauri. Asilimia 80 ya wananchi waliopimwa siku hiyo walikutwa na matatizo ya shinikizo la juu la damu na wengine walikutwa na matatizo mengine ya Moyo.
Aidha wagonjwa 400 waliokutwa na matatizo ya moyo walipewa dawa na baadhi yao walianzishiwa kliniki ili wataalamu wetu waweze kufuatilia maendeleo ya afya zao kwa ukaribu na kuweza kupata huduma ya matibabu kwa ukaribu zaidi.
Kwa namna ya kipekee tunazishukuru sana kampuni zinazotengeneza dawa za binadamu za Tata Africa Holdings (T) LTD, Reddy’s, na Phillips ambazo ziligawa dawa bure kwa wananchi waliokutwa na matatizo ya Moyo.
Tunawaomba wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wanamatatizo ya moyo au la na hivyo kuanza matibabu mapema. Asilimia kubwa ya wagonjwa tunaowapokea katika kliniki zetu baada ya kuwafanyiwa vipimo tunawakuta mioyo yao haiko katika hali nzuri. Hii inaonyesha kuwa wana matatizo ya Moyo pasipo kujifahamu.
Imetolewa na :
Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
04/10/2017
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...