Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo mjini Bagamoyo. Kushoto ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bi. Fransisca Muindi na Mkurugenzi wa Utumishi, Bi. Ediltruda Maseko.
Maafisa Rasilimali Watu wa TPA wakiwa katika semina hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko amefungua semina ya siku tatu (3) kwa Maafisa Rasilimali Watu wa TPA ambao wanafanyakazi katika maeneo mbalimbali ya Bandari hapa nchini.
Semina hiyo inayofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Wauguzi Bagamoyo inaenga kuwajengea uwezo Maafisa hao kuhusiana na masuala mazima ya Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...