Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Bohari ya Dawa nchini imewataka Wakurugenzi wa Halmashauri na Wenyeviti kuwasilisha mahitaji ya dawa na vifaa tiba vya Hospitali zao kabla ya tarehe 31 mwezi Januari kila mwaka,ili kuwasaidia kuharakisha hatua za manunuzi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wateja na Shughuli za Kanda MSD Daud Msasi alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa globu ya Jamii wakati kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (ALAT.

Msasi amesema kuwa Halmashauri zinapaswa kupeleka mahitaji halisi kulingana na bajeti walizonazo kwani kufanya hivyo itasaidia katika kupanga manunuzi ya vitu vinavyohitajika.

“Mahitaji yanatakiwa kuwahi kabla ya tarehe 31 mwezi wa kwanza. hii itasaidia sisi kwenda sokoni kwa wazalishaji na Viwandani hili kuweza kupata dawa kwa haraka” amesema Msasi.

Ameongeza mara baada ya tamko la Rais Dk John Magufuli kuagiza dawa zote ziagizwe na Bohari ya Dawa kwa sasa wameweza kupata dawa kwa bei raisin a zenye ubora unahohitajika.

Amesema kuwa licha ya MSD kuwa na mafanikio makubwa katika usambazaji wa dawa katika Halmashauri na Hospitali za mikoa pia mpango huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuepukana na ubabaishaji uliokuwa ukiletwa na watu wa kati.

Amemaliza kwa kutoa wito kwa Halmashauri zote nchini kusimamia vizuri vyanzo vyao vya mapato vinavyohusu huduma za afya hili waweze kulipa madeni yao kwa wakati.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za kanda -MSD ,Daudi Msasi akimuonesha mmoja wa Wateja vifaa tiba wakati wa Maonesho ya mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (ALAT)
Afisa Huduma kwa wateja MSD kanda ya Dar es Salaam Florida Siang'a akimuonesha bidha mmoja wa wateja waliotembelea banda lao katika Maonesho ya mkutano wa 33 wa Alat
Wafanyakazi wa Bohari ya dawa ya MSD wakito huduma kwa wageni waliofika katika mkutano wa 33 wa ALAT

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...