Na: Thobias Robert- MAELEZO

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa atashughulikia suala la rushwa pamoja na udanganyifu wa umri unaofanywa na baadhi ya watumishi wa umma hapa nchini.

Mkuchika aliyasema hayo Jijini Dar es Salaam katika mkabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo ambaye kwa sasa ni Waziri wa Madini, Angellah Kairuki katika ukumbi wa wizara hiyo.“Tutaongeza kasi ya kurejesha nidhamu, maadili na mapambano dhidi ya rushwa hapa nchini,” alifafanua waziri Mkuchika

Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro pamoja na watumishi wa wizara hiyo, Waziri Mkuchika alisema kuwa atahakikisha anashughulikia suala la watumishi kupandishwa madaraja pamoja na kuongezewa mishahara baada ya kukamilika zoezi la ukaguzi la watumishi hewa.

Aidha alisema kuwa suala la rushwa linatakiwa kujengewa msingi kutoka ngazi ya chini, hivyo ataongea na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ili kuweka somo la rushwa katika mitaala ya elimu hapa nchini kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu.
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye sasa amekuwa Waziri wa Madini Angelah Kairuki (kushoto) akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora George Mkuchika wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya ofisi leo jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni watumishi wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam katika hafla ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo Angellah Kairuki ambaye sasa amekuwa Waziri wa Madini 
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye sasa amekuwa Waziri wa Madini Angelah Kairuki akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari katika hafla ya kumkabidhi ofisi mrithi wake Waziri George Mkuchika leo Jijini Dar es Salaam .
Aliyekuwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angelah Kairuki akimkabidhi nyaraka za ofisi Waziri aliyeteuliwa kuongoza Wizara hiyo George Mkuchika katika hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angelah Kairuki akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari katika hafla ya makabidhiano ya ofisi na waziri aliyeteuliwa kuongoza wizara hiyo George Mkuchika leo jijini Dar es Salaam.Picha na: Thobias Robert – MAELEZO.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...