Na.Jacquiline Mrisho –
MAELEZO.
Serikali imetoa onyo
kali kwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mh. Zitto Kabwe juu ya taarifa za
upotoshaji wa takwimu za Pato la Taifa alizozitoa hivi karibuni.
Taarifa hizo za Mh.
Zitto zimeripoti kuwa ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwaka 2017
kuwa ni asilimia 5.7 badala ya asilimia 7.8. Kasi ya ukuaji ya asilimia 5.7
ilikuwa ni kwa robo ya kwanza ya Januari hadi Machi 2017.
Onyo hilo limetolewa leo
Jijini Dar es Salaam na Bw. Daniel Masolwa Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa
kutoka Ofisi ya Taifa za Takwimu (NBS),kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NBS,pamoja
na Mkurugenzi wa Sera na Tafiti za
Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw.Johnson Nyella wakati wakizungumza na
Waandishi wa Habari.
Masolwa amesema kuwa
upotoshaji huo uliofanywa na Mh. Zitto ni wa makusudi na unalenga kuonesha kuwa
juhudi znazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano hazina manufaa kwa Wananchi.
“Napenda kukanusha
kauli ya Mh. Zitto kuhusu taarifa zake zinazodai kuwa takwimu za Pato la Taifa
zimepikwa, Mh. Zitto anatakiwa kujua kwamba kazi ya kukokotoa takwimu za Pato
la Taifa ni ya kitaalam na inafuata miongozo inayotolewa na Kamisheni ya Umoja
wa Mataifa ya Takwimu na Shirika la Fedha Duniani (IMF)”,alisema Masolwa.
Meneja
wa Takwimu za Pato la Taifa toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel
Masolwa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo ichani)
wakati akikanusha taarifa za upotoshaji kuhusu takwimu za pato la taifa
mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na
Tafiti toka Benki Kuu Johnson Nyella
Mkurugenzi
wa Sera na Tafiti toka Benki Kuu Johnson Nyella (kushoto)akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo ichani) wakati akikanusha taarifa
za upotoshaji kuhusu takwimu za pato lataifa mapema hii leo jijini Dar
es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa toka Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel Masolwa.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...