NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAANDISHI wa habari ambao ni wanachama wa kundi la Whatsapp lijulikanalo kama TASNIA HALISI wamezindua kundi hilo Jumamosi jana Oktoba 28, 2017 kwa sherehe kabambe ya kukata na shoka iliyohanikizwa na nyama choma, vinywaji vya kila aina na muziki.
Mratibu wa shughuli hiyo Bi. Angela Msangi amesema kundi hilo ni mukusanyiko wa wanataaluma na wadau wa habari na linalenga kuwaleta pamoja wana tasnia kwa nia ya kubadilishana taarifa na kusaidiana kitaaluma na kijamii.
Katika uzinduzi huo umeshuhudia waandishi kutoka sehemu mbalimbali nchini wakishiriki, ambapo shampeni mbili zilifunguliwa pamoja na kukata keki.
Sehemu ya wanahabari wanachama wa kundi la Whatsapp la TASNIA HALISI wakifurahia wakati wa kuzindua kundi hilo Jumamosi jana Oktoba 28, 2017
Sehemu ya wanahabari wanachama wa kundi la Whatsapp la TASNIA HALISI wakifurahia wakati wa kuzindua kundi hilo Jumamosi jana Oktoba 28, 2017
Mratibu wa wa kundi la Whatsapp la TASNIA HALISI Angellah Msangi akiongea na Dennis Msacky wakati wa kuzindua kundi hilo Jumamosi jana Oktoba 28, 2017
Mdau mkuu wa kundi la Whatsapp la TASNIA HALISI Tedy Mapunda akifurahia wakati wa kuzindua kundi hilo Jumamosi jana Oktoba 28, 2017. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...