Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt Anna Peter Makalala ametoa zawadi kwa akina mama na watoto waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Temeke sambamba na kufanya usafi wa mazingira kuzunguka eneo hilo.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jhn Pombe Magufuli la kufanya usafi kila mwisho wa mwezi.
Kamishna Jenerali Anna alimkabidhi kijarida chenye masuala mbalimbali yanayohusu uhamiaji kwa mganga mkuu wa hospitali ya Temeke na kumtaka kushirikiana nao kwenye kutoa elimu kwa wagonjwa wanaofika hapo pale pindi wapatapo muda.
Mganga Mkuu wa hospitali ya Temeke Dr Amani Malima amewashukuru sana kwa kuja kufanya usafi kwenye hospitali hiyo na kutoa zawadi kwa wakina mama na watoto huku akiwahakikishia kuwa watatoa elimu kwa wagonjwa wanaofika hapo kuhusiana na masuala ya uhamiaji.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala akifanya usafi katika Hosptali ya Temeke ikiwa ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli ya kufanya usafi kila mwisho wa mwezi, usafi huo umefanyika kwa pamoja na wafanyakazi wa Uhamiaji Dar es Salaam Oktoba 28, 2017.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala pamoja na Mkuu wa Wilaya ya emeke Felix Lyaviva wakifanya usafi katika Hosptali ya Temeke ikiwa ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli ya kufanya usafi kila mwisho wa mwezi, usafi huo umefanyika kwa pamoja na wafanyakazi wa Uhamiaji Dar es Salaam Oktoba 28, 2017.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala akijadiliana jambo na mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaviva baada ya kuwasili katika Hospitali ya Temeke kwa ajili ya kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi kutii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli.
Kamishna Jeenerali akitoa zawadi ya pampers na sabuni kwa wakina mama waliojifungua watoto walio chini ya muda wake (njiti) walipowatembelea kwenye Hospitali ya Temeke walipokwenda kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala akitoa zawadi kwa wakina mama walipowatembelea kwenye Hospitali ya Temeke walipokwenda kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...