Na Mwandishi Wetu Tarime- Mara.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametoa miezi sita kwa Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kuanzisha Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto kwa ajili ya kusikilizamatatizo ya wanafunzi hasa wanafunzi wa kike.
Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa KikeKitaifa iliyofanyika katika wilaya ya Tarime mkoani Maraamewasisitiza wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kuzingatia uwepo wa dawati la ulinzi na usalama wa mtoto  kike katika shule zao ili kuwa salama na kuwa na mahali pa keleza matatizo yao.
Mhe. Ummy ameongeza kuwa suala la kumlinda mtoto wa kike ni jukumu la kila moja katika jamii na kuwapongeza wadau wa maendeleo ya watoto kwa jitihada zao na kushirikiana na Serikali kutoa elimu kwa wanajamii kuhusu madhara ya mimba za utotoni, ukeketaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua kampeni ya kitaifa ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” "Najitambua Elimu ndio Mpango mzima". 
 Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akibonyeza kitufe kuzindua ujumbe wa radio wa kampeni ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima” 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto, wadau na madereva bodaboda wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara muda mfupi baada ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika kitaifa wilayani Tarime mkoani Mara. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...