Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati akiwahamasisha wakazi wa Dar es Salaam kufika katika mbio za Kigamboni Marathon.
Na Agness Francis, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile, awataka wakazi wa wilaya ya Kigamboni pamoja na
wananchi wengine kutoka maeneo mbali mbali kujitokeza kwa wingi katika kushiriki tamasha la Mbio la Kigamboni Marathon, ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika kwa Kigamboni.
Dkt. Ndugulile amesema hayo leo katika Ofisi zake Jijini Dar Es Salaam kuwa mbio hizo ambazo huleta
manufaa kwa mwanadamu ambazo hujenga afya na mwili pamoja na kukutana na watu mbali
mbali wapya na kubadilisha mawazo ili kuleta mafanikio katika Wilaya hiyo mpya. amesema mbio hizo za Kigamboni Marathoni zitafanyika siku
ya jumamosi Disemba 2 mwaka huu kuanzia saa 12 asubuhi katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Mbio hizo zenye kilomita 21,10 hadi 5 zitakazoanzia darajani,feri kuelekea kibuguni hadi
kumalizikia katika ofisi za afisa wilaya ya kigamboni .
Pia amemalizia kwa kusema kuwa wanachi waendelee kujitokeza katika zoezi zima la kujaza fomu
ambazo zinapatikana katika ofisi za Mkuu wa wilaya wa Kigamboni ili kushiriki mbio hizo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile akipokea fulana kw ajili ya kushiriki Mbio za Kigamboni Marathoni
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...