Taasisi ya TradeMark, East Afrika itawasaidia wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuweza kufanya biashara ya kimataifa kwa kuyafikia masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hata nje ya Afrika. 
Ahadi hiyo, imetolewa na Mkurugenzi wa TradeMark  Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga (pichani), wakati akizungumzia mpango kamambe wa kuwasaidia wafanyabiashara wanawake wan chi 6 za Afrika Mashariki, uliozinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Nairobi nchini Kenya. 
Ulanga amesema, TradeMark East Africa, kupitia mradi wake wa “Women in Trade”  uliolenga kuwajengea uwezo wa wafanyabiashara wanawake kuhimili ushindani wa kibiashara na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiasha wanawake Tanzania kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa ikiwemo kuwezesha bidhaa zao kuyafikia masoko ya nchi za Afrika Mashariki na soko la kimataifa kwa kuanzia na wafanyabiashara wanawake wanaovuka mipaka ya nchi xa Afrika Mashariki. 

Bwana Ulanga amesema, TradeMark East Africa ni taasisi inayoongoza katika kuleta usawa wa kijinsia katika biashara, kwa sababu utafiti umeonyesha kuwa asilimia 70% ya wanaofanya biashara za mipakani ni wanawake na wanakabiliwa na vikwazo vingi vya kibiashara vikiwemo vikwazo vya kijiografia, vikwazo vya kijinsia, vikwazo vya kisheria, vikwazo vya kimtazamo, hivyo TradeMark imeandaa mpango kamambe wa miaka sita wa kuwajengea uwezo, atakaogharimu shilingi bilioni 12. 
TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, la maendeleo kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa njia ya biashara. TMEA inafanya kazi kwa karibu na taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.
 TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kwa kuongeza fursa za upatikanaji  wa  masoko, kuboresha mazingira ya biashara, biashara ya ushindani na kuongeza mchango wa biashara kuchangia ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini kwa kuleta maendeleo na ustawi wa jamii.

TMEA ina makao yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina  matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na Kigali.

Ili kujua zaidi kuhusu TMEA, tafadhali tembelea tovuti TMEA katika www. www.trademarkea.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...