NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said.
WAKATI
Mwaka 2017 ukifikia ukingoni taasisi mbaliombali nchini zimeanza kuwakusanya
watumishi wake na kufanya tathmini ya utendaji na kujadili namna ya kuzikabili
changamoto walizokutana nazo ili hatimaye kuongeza ufanisi mwaka ujao 2018.
Miongoni
mwa taasisi hizo ni Mwalimu Commercial Bank, (MCB), ambao wamekutana jijini Dar
es Salaam, ili kufanya tathmini ya kiutendaji na kuweka mikakati mipya
waingiapo mwaka 2018.
Wafanyakazi
hao kutoka idara mbalimbali wakiongozwa na Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald
Manongi pia walipatiwa semina kuhusu masuala mbalimbali ya kiuwajibikaji katika
maeneo tofauti kutoka kwa mtaalamu wa kujenga umoja kwa wafanyakazi ili kupata
matokeo bora, (Team building consultant), Elizabeth Wachuka.
Ili
kuonyesha ushirikiano wafanyakazi hao walibadilishana zawadi mbalimbali ambapo
kila mfanyakazi alimuandalia zawadi mfanyakazi anayemvutia zaidi kiutendaji.
Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...