Na Mwandishi Maalum, Tarime

Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Comrade Ngemela Lubinga jana (22/01/2018) ameanza ziara ya ukaguzi wa miradi ya TASAF mkoani Mara.

Ziara hiyo ni sehemu ya kufuatilia (monitoring) utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika mkoa wa Mara.Comrade Lubinga ameanza kwa kutembelea Wilaya ya Tarime ambapo alikutana na wanufaika wa Mpango wa TASAF wa kunusuru Kaya masikini katika Vijiji vya Gamasala Kata ya Nyandoto na Remagwe katika Kata ya Regicheri.

"Watendaji wa TASAF na wote wenye dhamana Serikalini, timizeni wajibu wenu na jitumeni zaidi katika kutatua changamoto za Wananchi wanyonge hawa na masikini ili nao wapate nafuu ya maisha," alisisitiza.

Vilevile, Comrade Lubinga amekemea tabia za ubadhilifu wa mali ya umma na kuonya kuwa watendaji wa aina hiyo hawana nafasi katika Serikali ya awamu ya tano chini ya Jemedari, Rais Dk John Magufuli."Serikali ya awamu tano iliyoundwa na CCM imedhamiria kuleta mabadiliko makubwa ya utumishi na kujenga nidhamu ya kazi katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania na hasusan wanyonge," alisema.

Ziara hiyo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa CCM katika kuisimamia Serikali yake kutekeleza Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2015. "CCM katika utaratibu wake wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ilani yetu, tumebaini changamoto katika mpango wa kupunguza umaskini na tumekuja kusikiliza kero za wananchi wetu ili kuzipatia majawabu," alisema Lubinga.

CCM mpya chini ya Mwenyekiti wake Dk John Pombe Magufuli, imeazimia kufuatilia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali ili kuharakisha maendeleo ya wananchi wake wakiokipa dhamana ya kuwaongoza, alisema. Ziara hiyo inaendelea leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...