Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameziagiza Halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa kuhakikisha zinafikia lengo la kupanda miti milioni 1.5 kila moja hadi kufikia mwisho wa mwaka wa 2017/2018 ili kufikia lengo la Mkoa la kupanda miti milioni 6 katika kutekeleza sera ya kupanda miti kitaifa.
Amesema kuwa Halmashauri itakayoshindwa kufikia lengo itatakiwa kulipa faini ya shilingi Milioni 1 kuilipa Halmashauri itakayofika lengo ambapo Halmashauri Mshindi inategemewa kupata shilingi Milioni 3 na fedha hizo itapewa taasisi itakayopanda miti mingi kuliko taasisi nyingine ya serikali ndani ya Halmashauri iliyoshinda hasa mashule ili kuwafundisha wanafunzi umuhimu wa kupanda miti.
“Halmashauri ambayo haikufikia lengo imuume kutoa shilingi Milioni 1 kumlipa mwenzake, katika hizo Halmashauri 4, kwa maana mshindi atapata shilingi Milioni 3, lakini endapo Halmashauri zote zitafikia malengo nitazipa Halmashauri Shilingi Milioni 1, na hiyo fedha itakwenda kwenye taasisi iliyopanda miti mingi kuliko taasisi nyingine hasa mashule,” Mh. Wangabo alibainisha.
Ameongeza kuwa mwaka ujao wa 2018/2019 halmashauri itakayoshindwa kufikia lengo la kupanda miti Milioni 1.5 italipa faini ya shilingi Milioni 5 ili kila halmashauri iweze kufikia lengo na kutimiza maelekezo ya serikali na kuwaonya wote wenye tabia ya kuchoma misitu jambo linalokwamisha jitihada za kutunza mazingira.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya REYO Abdallah Rubega (Flana Nyeupe) akitoa maelezo juu ya
aina ya miti itakayopandwa katika msitu wa Wangabo kwa heshima ya Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiwa katika picha ya pamoja na
wadau wa mazingira huku ameshikilia bango la kuhamasisha wananchi kuacha
kuchoma moto misitu na kuendelea kutunza vyanzo vya maji.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akipanda mti ishara ya kufungua
upandaji miti Mkoani Rukwa iuli kufikia lengo la mkoa la kupanda miti
milioni 6, Maadhimisho yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Matai,
Wilayani kalambo.
Mkuu
wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule (kulia) akisaidiana na baadhi
ya wananfunzi wa Shule ya Sekondari Matai kupanda miti ikiwa ni juhudi
za kuwaelimisha wananfunzi umuhimu wa kupanda miti.
Wanafunzi mbalimbali wakiendelea kupanda miti katika eneo lililoandaliwa maalum kwa kupanda miti katika shule hiyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...