Na Richard Mwaikenda, Msoga.
.RAIS mstaafu Dk.Jakaya Kikwete amefurahishwa na elimu ya kilimo cha kisasa cha Papai chenye gharama nafuu aliyopatiwa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Living green)
Elimu hiyo ilitolewa hivi karibuni nyumbani kwake Msoga, Chalinze, mkoani Pwani na Ezra Machogu Mtaalamu wa Kilimo wa Kampuni ya Awino Farm ambayo ni mwanachama wa Mkikita.
Kikwete alifurahi kuambiwa kwamba kampuni hiyo inaweza kuzalisha papai lenye ubora kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye gharama nafuu hivyo kumfanya mkulima apate faida kubwa wakati wa mauzo.
Ezra anasema kuwa unaweza kupunguza gharama kwa kuacha kuchimba mashimo badala yake unalima shamba mara tatu kwa kutumia trekta, hivyo kuufanya udongo kuwa tifutifu kitendo kitakacho kurahisishia kupanda miche ya papai bila matatizo.
Anasema ukitumia njia hiyo itakuondolea gharama ya kuchimba mashimo 1200 katika heka moja ambayo jumla ni sh. mil. 6 ikiwa kila shimo itakuwa sh. 500 wakati kulima mara tatu heka moja kwa trekta ni sh. 150,000.
Ezra anamweleza Dk. Kikwete kuwa unaweza pia kupunguza gharama ya mbolea kwa kila shimo kuweka majagi mawili badala ya debe moja.Pia alimweleza kuwa katika umwagiliaji papai halihitaji maji mengi, hivyo unaweza kutumia lita 10,000 kwa siku kumi badala ya siku nne.
Meneja
Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikwete, Justine (kushoto) akiwa na
Mkurugenzi wa Kampuni ya Awino, Martine Wamaya (kulia) na Mtalaamu wa
kilimo cha Papai, Ezra Machogu walipokuwa wakitoka kuchuma papai kutoka
kwenye shamba darasa la Kampuni ya Awino eneo la Msata tayari
kumpelekea Rais mstaafu, Dk. Kikwete.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...