Na Agness Francis Globu ya jamii.
KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imemfungulia mashitaka Mwenyekiti wa Abajalo FC na Mjumbe wa Bodi ya Ligi Edgar Chibula kwa tuhuma ya kuikashifu na kuidhalilisha Kamati ya Bodi ya Ligi ya TFF katika vyombo vya Habari ambapo ni kinyume na sheria.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,Ofisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema kuwa Chibura alishitakiwa Februari 28 mwaka huu kwa kosa la kuzungumza maneno yasiofaa kwa kuidhalilisha bodi hiyo katika vyomba vya habari ikiwa ni kinyume na kufungu cha sheria cha 50(1), (2) na (6) cha Katiba ya TFF toleo la mwaka 2015,pia ni kinyume na sheria kanuni za maadili toleo la 2013.
Aidha Ndimbo amesema kwenye shauri hilo mtuhumiwa huyo hakuhudhuria, isipokuwa alileta utetezi wake kwa njia ya maandishi
ambapo Sekretarieti ya TFF ilitoa ushahidi wa sauti(clip) ya mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha redio hapa nchini.
Ambapo kwenye mahojiano hayo mtuhumiwa alisikika akizungumza maneno hayo yasio na maadili katika maendeleo ya mpira wa miguu.
Ndimbo amesema kutokana na utovu wa nidhamu na kosa la kuzungumza maneno ya kuikashifu Bodi ya Ligi ya Mpira wa Miguu TFF, Kamati imeamua asijuhusishe na shughuli zozote za mpira wa miguu kwa kipindi cha mwaka mmoja pamoja na faini ya Sh.milioni 3 chini ya kufungu cha 73 (4) kanuni za maadili ya TFF toleo 2013.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...