Na Agness Francis, Globu ya Jamii.
MWENYEKITI wa Chama cha Soka cha Wanawake Tanzania Amina Karuma amewakumbusha viongozi wa timu mbali mbali za soka la wanawake zilizoingia 8 bora katika Ligi ya Serengeti Primer Lite kuzingatia sheria na kanuni 17 za Mpira wa Miguu.
Karuma amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Chichi Kinondoni wakati wa Semina elekezi kwa viongozi hao 24 huku akiwataka watambue wajibu wao kulea wachezaji wazuri ili kuisadia kufikia malengo ya kupata timu bora ya Taifa hapa nchini.
Aidha Karuma amesema wapo karibuni kuingia kambini na wanatarajia kucheza mechi ya kwanza na Zambia katika Kombe la Womes World ,
kabla ya kwenda kwenye challenge Cup nchini Rwanda kutetea ubingwa wao mara baada ya kuwasiliana na Baraza la Soka la Afrika. Mashariki na Kati (CECAFA)
Hata hivyo, Karuma amesema licha ya wachezaji kujitahidi, ametoa mwito kwa wadhamini waendelee kujitokeza kufadhili timu hizo ili kusaidia kuleta maendeleo ya soka la wanawake hapa nchini.Kwa upande wa Kocha Mkuu Aliance Girls Ezekiel Chobaka amezungumzia utendaji mzuri wa timu yake tangu alipoanza rasmi kuifundisha Mei 5 mwaka jana.
"Maendeleo ni mazuri kwa timu yangu na ninamatumaini kufanya vizuri katika Ligi Kuu, vilevile tumeweza kuchukua ubingwa katika Ligi kuu Mkoa wa Mwanza," amesema Chabaka.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Wanawake Tanzania, Amina Karuma akizungumza na Viongozi wa Timu zilizoingia 8 bora ya Ligi ya Serengeti Primer Lite katika semina elekezi iliofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika.
Viongozi mbalimbali wa Timu hizo zilizoingia 8 Bora Ligi ya Wanawake Serengeti Premier Lite wakisikiliza mafunzo na maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Wanawake Tanzania, Amina Karuma leo Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...