Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MBUBGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete(CCM),amesema migogoro ya ardhi ni moja ya Changamoto kubwa inayotukabili wana Chalinze.
Akizungumza leo na Michuzi Blog amesema kutokana na changamoto hiyo jana ameamua kufanya ziara katika Kijiji cha Kwamduma, Kata ya Kibindu kuangalia athari za migogoro baina ya kijiji na Hifadhi ya Uzigua.
Amesema katika ziara hiyo ameona hitaji la kukaa chini na watu wa hifadhi kwa lengo la kujadili suala la mipaka inayotembea." Tumekubaliana na Serikali kuingilia hili jambo mara moja na imekubali kulishughulikia ndani ya kipindi kifupi,"amesema Ridhiwan.
Ameongeza kuwa ataendelea kushirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali na wananchi wa Chalinze ili kupata ufumbuzi wa migogoro ya ardhi ndani ya jimbo hilo.
"Kazi zinazoacha alama, Chalinze ni kazi tu,CCM ni kazi tu, Magufuli ni kazi tu, Kwamduma ni kazi tu na Kibindu ni kazi tu,"amesema Ridhiwan baada ya kufanya ziara hiyo na kuongeza ataendelea kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Chalinze.

Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete akiangalia mipaka katika kijiji cha Kwamduma jana akiwa na baadhi ya viongozi wa kijiji .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...