Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa dini ambapo katika kikao hicho kamati ya Amani ya Mkoa imeundwa ikihusisha viongozi wa Dini zote. Katika kikao hicho masuala mbalimbali ya maendeleo yamejadiliwa pia, na amewashukuru viongozi hao kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuliombea Taifa na kukemea maovu. RC Mndeme amewaomba viongozi hao wa dini kuendelea kuliombea Taifa na pia ameahidi kuwapa ushirikaiano mkubwa kwa maendeleo ya Ruvuma na Taifa kwa ujumla pia kukemea maovu miongoni mwa jamii.
Kwa upande wao viongozi wa dini wamemshukuru mkuu wa mkoa kwa hatua hiyo waliyoiita ya kihistoria, na wameahidi kushirikiana naye pamoja na serikali bega kwa bega ili kujenga jamii yenye kujali utu, maadili na inayochukia maovu.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme Mhe. leo katika picha ya pamoja na viongozi wa dini ambao wanaunda kamati ya Amani ya Mkoa wa Ruvuma baada ya kikao chao.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme Mhe. leo akiwa na iongozi wa dini wanaounda kamati ya Amani ya Mkoa wa Ruvuma pamoja na wadau na maafisa kutoka katika ofisi yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...