Na John Mapepele

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Joelson Mpina amekamata marobota 1152 ya aina mbalimbali za nyavu haramu zisizoruhusiwa kisheria kutumika kuvulia samaki zenye thamani ya shilingi milioni 894 jijini Mwanza na Singida ambapo baadhi ya nyavu hizo zimetaifishwa na nyingine kuteketezwa na wamiliki wakitakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 120 ndani ya masaa 24 kwa makosa ya kufanya biashara ya nyavu hizo kinyume cha sheria.

Akiongea na Vyombo vya Habari jijini Mwanza katika ghala la nyavu la Meshack Chacha mara baada ya kukamata shehena ya marobota 600 ya nyavu haramu kwenye ghala lake, Mhe. Mpina alisema nyavu haramu 294 kati ya 894 zilikamatwa na kikosi kazi maalum cha kudhibiti uvuvi haramu katika kanda ya Ziwa Victoria alichokiunda hivi karibuni wakati mmoja wa wafanyabiashara hao Masagati Majani alijaribu kutorosha vyavu hizo kwa kutumia gari aina ya Scania lenye namba za usajili T.452 BBS kutoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam.

Gari hilo lipo katika kituo cha polisi cha Singida kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ambapo kulingana na sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003, imetoa mamlaka kwa watendaji wa Serikali kutaifisha mali zote zilitumika katika uvuvi haramu kupitia kifungu cha 37(a) (ii) na (iii)

Aliwataja wamiliki wengine ambao walikamatwa kutokana na kujihusisha na biashara haramu ya uagizaji na uuzaji wa vyavu zisizoruhusiwa kisheria kuwa ni Josia Jonam Obielo, Jeremiah Asam na Dastun Venant ambapo alisema Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba wafanyabiashara wote wanao agiza na kuuza zana haramu za uvuvi wanakamatwa na sheria kali zinachukuliwa ili kudhibiti uvuvi haramu nchini.

“Niliapa kusimamia ulinzi wa raslimali za uvuvi nchini hivyo nitahakikisha operesheni hii inakuwa ya kudumu katika kupambana na uvuvi haramu hadi uvuvi haramu utakapokwisha” alisisitiza Mpina

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina(mwenye kofia) akiwa na Kiongozi wa Operesheni ya maalum ya kudhibiti uvuvi haramu katika ukanda wa Ziwa Victoria, Shafii Ramadhani Kiteri wakikagua shehena ya marobota 600 ya nyavu haramu zenye thamani ya shilingi milioni mia tano inayomilikiwa na Meshaki Chacha jijini Mwanza leo. Nyavu hizo zimetaifishwa na nyingine kuteketezwa na mmliki akitakiwa kulipa faini ya shilingi milioni hamsini ndani ya masaa 24.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani na kofia )akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ukerewe, Frank Bahati (kushoto) wakiwa kwenye boti ya doria kutoka katika kijiji Kakukuru wakielekea kwenye kambi ya uvuvi ya Kisiwa cha Galinzila ambapo Mhe.Waziri alifanya mkutano na wavuvi . Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomiah Chang’a. (Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani)akikagua nyavu haramu za kuvulia samaki katika kijiji cha Kakukuru wilayani Ukerewe ambapo alichoma moto nyavu haramu za zenye thamani ya shilingi bilioni mbili. Kulia ni Lameki Mongo, Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kushoto ni Abbakary Murshidi, Afisa Uvuvi wa Wilaya ya  Ukerewe (Na John Mapepele) Aapa kutokomeza uvuvi haramu nchini
Asema imebaki 3% tu ya Sangara wanaokubalika kuvuliwa katika ziwa Victoria .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...