Baada ya kufanyika michuano ya Sports Xtra Ndondo Cup kwa mafanikio katika mikoa ya Mwanza na Mbeya sasa yaongeza wigo kwa mabingwa wa mikoa.
jana jijini Mbeya kamati ya mashindano hayo imetangaza rasmi uwepo wa mashindano ya Ndondo Super Cup itakayofanyika jijini Dar es salaam mwezi februari kwa kushirikisha mabingwa wa mikoa ilipofanyika Sports Xtra Ndondo Cup.
Mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Cup Shaffih Dauda amewaambia waandishi wa habari kuwa uwepo wa mashindano hayo ni hitimisho la msimu wa Ndondo Cup 2017 kabla ya kuzinduliwa msimu mpya mwezi wa tatu. "Mashindano hayo yatashirikisha timu nne na kutakua na michezo minne itakayofanyika tarehe 17, 18, 20, na 21 mwezi februari jiji Dar es salaam" amesema Dauda.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Super Cup Gipson George amesema hili ni jambo lingine kubwa kutoka Clouds Media kama support ya wanamichezo wa Tanzania na ulimwenguni kote kwa ujumla hususani ujio wa viongozi wa FIFA nchini. "Hakuna asiyejua Rais wa FIFA atakuwepo hapa, hii ni heshima kubwa tuliyopewa Duniani lazima na sisi tuwaoneshe kuthamini ujio wao"
"Shaffih Dauda amewasiliana na TFF kuona namna ya kushirikiana kutusaidia kuwezesha kumpata rais wa FIFA kuja kwenye fainali ya Ndondo Super Cup ndio maana tumepanga iwe tarehe 21" amesema Gipson.
Gipson ameongeza kuwa mashindano hayo yanaendana na agenda ya Rais wa sasa wa FIFA ya kurudi chini kabisa (grassroot) mpira unapochezwa na watu wa kawaida wenye vipaji vya hali ya juu. Msafara wa FIFA ukiongozwa na Rais Infantino unatarajiwa kuwasili nchini tarehe 21 na siku inayofuata watakua katika mkutano utakaofanyika hapa nchini.

Mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Cup Shaffih Dauda akifafanua jambo kwenye mkutano huo uliofanyika mapema jana jijini Mbeya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...