Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

WAFITI mbalimbali nchini wakiongozwa na Taasisi ya Utafiti Repoa  wamekuta jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili masuala yanayohusu tafiti huku moja ya mada ikiwa ni namna gani watakabiliana na changamoto ya kupotoshwa kwa tafiti kutokana  na kukua kwa teknolokia na hali ya kisiasa.

Mbali ya watafiti wa Tanzania, pia watafiti wa nchi zaidi ya 170 duniani nao wamekutana kwenye mkutano maalumu kama ambao umefanyika nchini kujadili masuala hayo hayo yanayohusu tafiti na changamoto zake.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Repoa Dk.Mmari amesema kukutana kwao kwenye mkutano huo unalenga kuzungumzia umuhimu wa taasisi za utafiti duniani ambapo kwa mwaka huu wanazungumzia changamoto ya ukuaji wa teknolojia na watu kupotosha tafiti kutokana na hali ya kisiasa.

"Mkutano huu unafanyika pia kwenye nchi nyingine 170 duniani.Moja ya ajenda ni hii ya changamoto ya ukuaji wa teknolojia na watu kupotosha tafiti kutoka na hali ya kisiasa.Mkutano huu unajulikana "Why thinks matter "na umeanza saa tatu asubuhi hadi saa tano kwa nchi zote hizo,"amesema Dk.Mmari.

Dk. Mmari amefafanua siku hizi kuna changamoto ya mitandao ya kijamii kwani taarifa zinasambaa kwa haraka na nyingine hazina ukweli wowote na kusababisha viongozi kuziamini na kuzitumia katika utungaji wa sera na kuendesha shughuli za Serikali."Hivyo imeonekana ni muhimu mwaka huu wakazungumzia tafiti ambazo zimefanyiwa kazi kisayansi,"amefafanua Dk.Mmari.

Ameongeza umuhimu wa watafiti na utafiti umesaidia katika kufanya maendeleo ya kweli ,hivyo amewahimiza Watanzania kuendelea kufanya tafiti zitakazotumika kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya Serikali na wadau mbalimbali."Si vyema watafaiti wakafanya tafiti ambazo zinawekwa  tu kwenye makabati pasipo kuwa na matokeo yoyote chanya kwa Taifa,"amesema Dk.Mmari.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti Nchini,REPOA, Dr Donald Mmari  akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Tafiti Duniani ambao kwa Tanzania ulifanyika katika Ofisi za Repoa na kuitwa jina la Umuhimu wa Tafiti Duniani
 Balozi wa Swideni Nchini, Katarina Rangnitt akizungumza wakati wa Mkutano wa Watafiti Duniani(WHY THINK TANKS MATTER) uliofanyika katika Taasisi ya utafiti ya Repoa kwa hapa nchini.
 Mtafiti Kutoka Tasisi ya Utafiti ya Repoa,  Dr Blandina Kilama akizungumza wakati wa mkutano huo wa watafiti Duniani.
 Baadhi ya Maprofesa walioshiriki Mkutano huo wakiongozwa na Profesa Mwesigwa Baregu wa kwanza kulia Pichani.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano huo wakisikiliza Mada Mbalimbali kutoka kwa watafiti  na Wadau mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...