Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

WATU saba wakazi wa sehemu tofauti jijini Dar es Salaam,wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuiba roli nne za waya za umeme zenye thamani ya Dola za Marekani 52268.78 sawa na Sh.116,872,813 mali ya  Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco).

Mwendesha mashtaka wakili wa Serikali, Herieth Lopa amewataja washtakiwa hao kuwa ni Mbatia Mhando (35), Abdallah Tambwambwa (39),  Willy Mgimbudzi (32), Francis Nchimbi (50), Ally Mohammed (42), Hassan Haji (29) na Misana Selestine (27).

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu mkazi Mkuu, Huruma Shaidi Wakili Lopa amedai, Desemba 16 mwaka 2017 huko Tabata Kinyerezi washtakiwa hao waliiba roli hizo nne za nyaya za umeme zenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Wakili huyo wa Serikali alidai katika kipindi hicho,washtakiwa kwa vitendo vyao na kwa makusudi walisababisha hasara ya Sh 116,872,813 mali ya Tanesco.Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kuzungumza chochote kwa sababu Mahakama haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Kesi imeahirishwa  hadi Februari 7, mwaka 2018.Katika kesi nyingine, Peter Mdegera na Ali Mayumba wamefikishwa mahakamani hapo,kujibu tuhuma za kukutwa na kilo 192.46 za dawa za kulevya aina ya bangi.Wakili wa Serikali, Lopa amedai mbele ya Hakimu Shaidi kuwa  Septemba 7, mwaka 2017 katika Mtaa wa Tarangile Mbezi Beach washtakiwa hao walikuwa wakiwa bangi hizo.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu ya Tanzania.Hata hivyo baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, mshtakiwa Ali alieleza mahakamani hapo kuwa anaumwa mguu kwa kuwa alipigwa na askari na kwamba kutokana na kipigo hicho sehemu zake za siri za kiume azisimami hivyo anahitaji msaada wa matibabu.

Mbali na Ali na mshtakiwa mwenzake Peter anaye alilalamika kuwa naye alipigwa.Baada ya kuwasikiliza washtakiwa hao, Hakimu Shaidi aliwaeleza wakipelekwa gerezani watapatiwa matibabu na kama hawatapatiwe tarehe ijayo watoe taarifa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februairi 7,2018 washtakiwa walipelekwa rumande.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...