Na Dotto Mwaibale

KUFUATIA agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli, kwa Wizara ya Kilimo, kuhakikisha ndani ya siku saba kumaliza malalamiko ya mahitaji ya mbolea kwa mikoa ya Katavi na Rukwa, Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC) imeanza mara moja kuteleleza agizo hilo.

Waandishi wa Habari jana na leo wameshuhudia watendaji wa TFC wakihaha kutafuta magari ya kukodi kwa ajili ya kusafirisha mbolea kuipeleka mkoani Rukwa na Katavi, ambapo zaidi ya tani 600 zimeanza kusafirishwa kuanzia juzi siku ya agizo hilo.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Salum Mkumba, alisema mara baada ya taarifa ya Ikulu juzi, waliamua kuanza kupakia mbolea hiyo, kwa kutumia magari makubwa (malori) ya kukodi pamoja na magari makubwa ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

“Kwa sasa sisi TFC hatuna akiba ya mbolea, lakini hawa wenzetu wa Primium Agro Limited, wanayo akiba ya kutosha, hivyo tunachukua kwao kwa makubaliano maalum,” alisema Mkumba.




Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC), Salum Mkumba (kushoto), akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Premium Agro Chem Limited inayosambaza mbolea alipofanya ziara ya kikazi ya siku mbili jana na leo jijini Dar es Salaam kujionea zoezi la kusafirisha mbolea kwenda mikoani. Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Brijesh Barot, Mkurugenzi Mtendaji, Sagar Shah na Oparesheni Meneja, Rhoda Mwita.
Wafanyakazi wa kampuni hiyo na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakipakia mbolea hiyo kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda mikoani.
Malori ya JWTZ yakiwa katika foleni ya kupakia mbolea hiyo.
Shehena ya mbolea hiyo ambayo inasafirishwa kwenda mikoani kwa wakulima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...