Na Agness Francis, Globu ya Jamii
VIONGOZI wa tatu wa ngazi za juu katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) wanatarajia kuhudhuria mkutano mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika(CAF).
Taarifa ya TFF iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam imesema mkutano huo utafanyika Februari 2 mwaka huu nchini Morocco.
Imesema viongozi watakaohudhuria ni Rais wa Bodi ya Ligi ya Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia, Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura na Kaimu mkuu wa Bodi hiyo Kidao Wilfred.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...