Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii .
MSHINDI wa Miss Tanzania mwaka 2012 Brigita Alfred ameweataka wadau wa masuala ya urembo na mitindo kuacha kubagua watu kutokana na mapungufu yao ya kimaumbile katika tasnia hiyo.
Brigita amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akitoa neno la shukrani kwa wadau wa mitindo na urembo waliofika katika onesho lake Maalum kwa watu wenye ulemavu wa ngozi lililofanyika nyumbani kwa Balozi wa Uturuki lililokwenda kwa jina la 'My Skin My Pride' na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
" Unaweza ukaona ukadhani labda nimefanya haya maonesho kwa ajili ya tasisi yangu lakini ukweli unabaki palepale kuwa katika tasnia ya mitindo sasa tunapaswa kuwapa nafasi watu wenye matatizo ya ulemavu wa ngozi kuonesha vipaji vyao na uzuri wa ngozi yao kuliko kuwaacha wenyewe jambo linalo wafanya wajisikie tofauti"amesema Brigita.
Amesema ni jambo zuri sasa kwa waandaaji wa mashindano ya urembo na mitindo kuwajumuisha wadau hao hili nao waonekane katika majukwaa ya kimataifa.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Brigita Foundation, Brigita Alfred akizungumza
kwa kuwashukuru wadau mbalimbali waliofika wakati wa Fashion Show ya
watu ya wenye ulemavu wa ngozi iliyofanyika nyumbani kwa balozi wa
Uturuki Masaki jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wana Mitindo mwenye ulemavu wa ngozi akiwa anapita jukwaani akionyesha mavazi yaliyobuniwa na wanamitindo mbalimbali
Warembo waliowahi kushika taji la Miss Tanzania nchini Nancy Sumari na
Jackline Mengi wakishuhudia onesho hilo la mitindo kwa watu wenye
ulemavu wa ngozi.
Mwanamitindo
Nemalisa akiwa na Mmoja wa warembo wenye ulamavu wa ngozi akionyesha
Vazi la nguo za jioni lililoandaliwa na kampuni ya Jackies Collection.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...