Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
WAFANYAKAZI wa kampuni ya udalali ya Tambaza jijini Dar es Salaam, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 40,000 kwa mwendesha pikipiki( bodaboda).
Washitakiwa hao, Christopher Mbiku na Deus Warioba ambao wamesomewa mashitaka yao leo mahakamani hapo na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), Leornad Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa,
Imedaiwa Januari 23 mwaka huu, maeneo ya Daraja Salender Bridge wilayani Ilala, Dar es Salaam washtakiwa walishawishi kupewa rushwa ya Sh.40,000.
Alidai kuwa washitakiwa walishawishi fedha hizo kutoka kwa Abul Malenda ambae ni dereva wa bodaboda kwa madai kwamba hawatamchukulia hatua za kisheria kutokana na kosa la kutokuwa na kadi na kibali cha kuendesha pikipiki mjini kitendo ambacho ni kinyume na taratibu.
Pia alidai Januari 23, mwaka huu maeneo hayo hayo, washtakiwa hao walipokea rushwa ya Sh.40,000 kutoka kwa Malenda kwa madai wasingemchukulia hatua za kisheria kwa kutokuwa na kadi na kibali cha kuendesha pikipiki na mjini.
Katika mashitaka ya tatu inadaiwa, Januari 23, mwaka huu maeneo hayo ya daraja la Salander wilayani Ilala, washitakiwa wote kwa pamoja walijipatia sh. 40,000 kwa njia ya udanganyifu kwa kujitambulisha kuwa wao ni watumishi wa Kampuni ya udalali ya Tambaza kitu ambacho si kweli.
Washitakiwa walikana mashitaka na wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi Februari 23 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo umekamilika ambapo upande wa mashitaka umeomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...