Said Mwishehe, Blogu ya jamii

SERIKALI imewataka watendaji na watumishi wa umma kuhakikisha wanakwenda na dhamira ya Rais, Dk.John Magufuli ya Hapa Kazi Tu, kinyume na hapo watachukuliwa hatua za kiutendaji.

Hayo yamesemwa leo, Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi wakati akifafanua mambo mbalimbali yanayoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa maslahi ya Watanzania wote.

Dk.Abbas amesema ni vema watendaji wa Serikali wakaenda sawa na dhamira ya Rais ya Hapa Kazi Tu, hivyo lazima wafanye kwa bidii na kufafanua kila mtendaji wa umma ajitafakari namna ya utendaji kazi wake kama unaendana na kasi ya Rais.

“Watendaji wa umma wajitafakari kuhusu kazi wanazofanya kama zinaenda na dhana ya Rais wetu ya Hapa Kazi Tu.Watendaji watimize majukumu yao na kufuatilia kila jambo kwani wasipofanya hivyo wapo watakaowafuatilia.

“Kuna mabadiliko makubwa ya kiutendaji kwa Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo lazima twende nayo.Tuhakikishe tunafanya kazi ili kufanikisha maendeleo ya Watanzania,”amesema

Dkt.Abbas ameamua kueleza hayo baada ya kuulizaa bado wapo watendaji ambao hawaendani na dhamira ya Rais ya Hapa Kazi Tu, Je wanawafanya nini watendaji kama hao.Wakati huohuo Dkt.Abbas ameendelea kuviomba vyombo vya habari kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia taaluma ya habari inavyotaka.

Amesema yeye kama mlezi wa vyombo vya habari nchini anayo nafasi ya kuendelea kushauri waandishi wa habari nchini kufanya kazi yao kwa kuzingatia misingi ya taaluma ikiwa pamoja na kuandika habari sahihi na iliyokamilika.Amefafanua njia pekee ya kuwa salama kwa vyombo vya habari ni kuandika ukweli badala ya kuandika mambo ya kuzusha au kuandika uongo kwani madhara yake ni makubwa.

”Binafsi kama mlezi wa vyombo vya habari lazima nikumbushe yale ambayo najua ni muhimu kuyazingatia.Pale ambapo kuna chombo kitakosea lazima tukiite na kukionya na tunafanya hivyo zaidi ya mara moja.
Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati alipotoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kutolea ufafanuzi wa masuala kadhaa, Pichani kushoto  Mkurugenzi Msaidizi upande wa usajiri wa Magazeti Ndugu Patric Kipangula  na Kulia Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo, Rodney Thadeus .PICHA NA MICHUZI JR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...