Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage afanya Ziara katika
mkoa wa Simiyu leo tarehe 2/1/2018.
Katika ziara yake Mhe. Mwijage amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony
Mtaka na kufanya mazungumzo mafupi kabla ya kushiriki zoezi la ufunguzi wa ofisi za
SIDO mkoa wa Simiyu.
Mara baada ya Ufunguzi wa Ofisi hizo Mhe. Waziri alipata furesa ya kuzungumza
machche na kutoa maagizo ya Utekelezaji. Kwanza alianza kwa kuupongeza uongozi wa
SIDO kwa kujenga Ofisi hizo ambapo ameagiza kuwepo madarasa maalumu ya
mafunzo kwa vitendo.
Mhe. Waziri amesema “Uchumi wa Viwanda utajengwa na Viwanda vidogo hivyo
Uzinduzi wa ofisi hizi za SIDO ndio chachu ya maendeleo ya Viwanda katika Mkoa wa
SIMIYU”. Aidha Mhe. Waziri alitembelea eneo la Viwanda na kukabidhi eneo hilo kwa Mkandarasi
ambaye anatakiwa kujenga kwa haraka ili watanzania wapate fursa ya kuanzisha
Viwanda.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jingo la ofisi za SIDO Mkoa wa Simiyu.
Pia Waziri alihitimisha ziara yake kwa kuklutana na Viongozi wa Serikali, Vipongozi wa
Dini, Viongozi wa Vyama, Wawekezaji na Wafanyabiashara na kuzungumza nao juu ya
Serikali ya awamu ya tano ilivyojipanga katika kuendeleza Viwanda nchini.
Mhe. Waziri alieleza kuwa, wananchi wa Mkoa wa Simiyu sasa watapata fursa za
kuwekeza, kufanya biashara, waatapata ajira pamoja na mikopo nafuu mara baada ya
ujenzi wa eneo la Viwanda.
Mhe. Waziri alieleza kuwa kujenga uchumi wa Viwanda ambao ni shughuli ya kiujumla
inayomtaka kila mmoja kushiriki katika kuhakikisha tunafanikisha adhma ya kuwa nchi
ya Viwanda ifikapo mwaka 2025. Pia aliongeza kuwa Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji ndiyo injini ya mafanikio katika uchumi kwa vile uchumi wa nchi yoyote
hubebwa na Viwanda ambavyo huzalisha bidhaa zitokanazo na malighafi zinazozalishwa
sehemu husika na kutumika katika eneo husika.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, akiwa katikla eneo litakalojengwa Viwanda.
Mhe, Waziri amesema kuwa tunataka nchi yetu tujivunie bidhaa zinzozalishwa nchini
kwa kuhamasisha kila mwananchi kupenda na kununua bidhaa Bidhaa za Tanzania kwa
sasa zinakubalika Supermarket nyingi kwa kuwa zinakidhi ubora kupitia TBS na TFDA,
aliongeza kwa kusema kuwa Kiwanda ni uongezwaji thamani kutoka malighafi na kuwa
bidhaa ambapo Lengo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli ni kuwa na Viwanda vingi vizalishe bidhaa bora ili tuuze katika
masoko ya ndani na nje ya nchi.
Mhe. Waziri amesema kuwa Wawekezaji na Wafanyabiashara kujifunza na kuzoea
kufanya uwekezaji unaokubalika kisheria (Legal Business Practices) fuateni taratibu za
nchi, kulipa kodi zinazowahusu na kuzalisha bidhaa bora na Serikali itasaidia kurahisha
shughuli zao.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Viongozi wa dini pamoja, wafanyabiashara na wawekezaji waliohudhuria mkutano huo, pembeni ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Athony Mtaka.
Pia Mhe. Waziri amehimiza Matumizi ya Teknolojia kwa maendeleo ya biashara ambapo
amesema ni muhimu kwa wawekezaji hasa wa ndani kwenda sambamba na mahitaji ya
teknolojia katika kuzalisha na kuuza bidhaa.
Mhe. Waziri amemaliza kwa kusema kusema kuwa Serikali imewekeza nguvu kubwa
kwa SIDO katika ujenzi wa Viwanda nchi nzima ambapo Wizara inapokea changamoto
mbalimbali zinazokwamisha biashara zao na kuzifanyia kazi kupitia anuani ya
dawatilamsaada@mit.go.tz
Mhe. Waziri ataendelea na ziara yake kesho Tarehe 3 Januari, 2018 katika Mkoa wa
Geita.
Viongozi wa Serikali na Wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano wa Mhe. Waziri katika ukumbi wa
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambapo mambo mbalimbali yalijadiliwa.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akivalishwa scarf ya heshima
kutoka kwa Vijana wa Skauti wa Mkoa wa Simiyu.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...