Wizara ya Maliasili na Utalii kuikarabati nyumba ya Nyerere Magomeni-Dk Kigwangalla Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla (MB) mapema leo Januari 26,2018,amefanya ziara maalum katika Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda Namba 62, ambayo aliishi hapo miaka ya 1950's .

Dk. Kigwangalla ameweza kujionea mambo mbalimbali ndani ya makumbusho hayo huku pia akipokea maoni ya namna ya kufanyiwa maboresho ya kituo hicho ikiwemo ufinyu wa eneo la ofisi na maegesho ya wageni wanaotembelea hapo.

"Nimefika hapa leo kujionea Kituo hichi ambacho ni kielelezo kikubwa cha Mwasisi wa Taifa letu. Hapa pana hazina kubwa na kituo hiki kina mambo mengi sana ya kumuenzi Baba wa Taifa. Kwa hali tuliookuta kwa kweli tutakaa na timu yangu kuona tunafanya maboresho makubwa kabisa ili kiwe kama maeneo mengine yenye Wahasisi wa Mataifa yao, tumeona kama eneo alilozaliwa Mzee Mandela kule Afrika Kusini, nyumba yake imehifadhiwa vizuri na imekuwa na wageni wengi. Kwa hapa kwetu na sisi tutakaa na wenzetu kutatua changamoto hizi. 

Hapa tutajenga Maktaba ambapo watu watakuja kusoma vitabu vya Mwasisi wetu na kuona mambo aliyokuwa akifanya. Lakini pia tutaonana na Viongozi wa Halmashau ri ya Kinondoni kuona namna ya kupaboresha mahala hapa ikiwemo miundombinu ya Barabara ya kuingia na kutoka eneo ili" alieleza Dk. Kigwangalla.
  
Muhifadhi Mkuu wa Makumbusho nyumba ya Nyerere iliyopo Magomeni Jijini Dar es Salaam,Bi. Neema Mbwana akisoma taarifa za kituo hicho kwa Waziri Dk Kigwangalla alipotembelea kituoni hapo mapema leo Januari 26,2018.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Kigwangalla akisaini kitabu cha Wageni alipowasili kituoni hapo
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Kigwangalla akitambulishwa wafanyakazi wa kituo hicho
Dk. Kigwangalla akitazama baadhi ya vitabu vya Mwalimu Nyerere ambavyo vimehifadhiwa nyumbani hapo
Dk. Kigwangalla akitazama baadhi ya picha mbalimbali za Baba wa Taifa ambazo zipo nyumbani hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...